Supu ya Samaki Mchanganyiko - ChefMapishi.

Mahitaji

  • Samaki
  • Kitunguu maji 1
  • Kitunguu saumu, punje 3, menya kisha saga.
  • Karoti 1
  • Pilipili hoho 1
  • Kabichi ½
  • Mbegu za Koriandaa kijiko 1 kidogo
  • Viazi mbatata (mviringo) ¼ kilo, au unaweza kutumia ndizi mbichi
  • Kiungo cha mboga, mie nimetumia royco

Maelekezo

  • Andaa samaki – toa magamba, toa utumbo na uchafu. Osha kisha weka samaki kwenye sufuria. Kama samaki mkubwa sana unaweza kumkata vipande vidogo ili atoshe kwenye sufuria na aive vizuri.
  • Menya kisha Kata kitunguu maji, karoti, na pilipili hoho. Weka kwenye sufuria yenye samaki. Kata kabichi kwenye vipande vya wastani, ongeza kwenye sufuria yenye samaki.
  • Menya viazi au ndizi kisha kata vipande vya wastani. Weka pia kwenye sufuria yenye samaki.
  • Weka kitunguu saumu na curry powder. Unaweza kuweka pilipili unazopenda ili kuleta ladha nzuri ya supu. Weka maji kidogo na chumvi kwenye sufuria. Bandika sufuria jikoni acha ichemke. Viazi vikianza kuiva, ongeza maji kiwango unachotaka cha supu.
  • Weka kiungo cha mboga, nimetumia royco, kama kijiko 1 kikubwa na mbegu za korianda. Funika na acha supu ichemke hadi uone ibaki kiwango unachotaka. Epua na tenga pembeni.
Unaweza kula supu hii kama yenyewe, kwa mkate, mihogo, maandazi, au chochote unachoamua. Tenga supu na ujirambe kwa raha zako

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post
Ads1
Ads2