Mahitaji
- Ulimi wa ng'ombe
- Soya sauce
- Ndimu
- Kitunguu saumu
- Chumvi
- Pilipili mbuzi
- Karoti
- Maji
Maelekezo
- Nunua ulimi ambao umeshatengenezwa kabisa.
- Bandika sufuria jikoni, weka ulimi, weka chumvi, kamulia ndimu, weka vitunguu saumu na karoti.
- Kata karoti vipande vidogo na vyembamba.
- Weka maji ya kutosha .Funika Sufuria na mfuniko.
- Ikikaribia kuiva weka soya sauce, hii inasaidia kuongeza ladha kwenye supu.
- Onja kama nyama imeiva, kama tayari weka pilipili. Vilevile unaweza kuongeza pililipi ukishaipua supu toka jikoni.
NB: Kuongeza pilipili pembeni
itasaidia kuwafanya hata wale wasiotumia pilipili kunywa supu bila
kupata adha ya ukali wa pilipili
- Hapo utakua tayari kujiramba na supu ya ulimi wa ng'ombe.
Post a Comment