Mahitaji
- Samaki 2
- Ndizi (aina yeyote, katika mapishi haya nimetumia ndizi bukoba)
- Karoti
- Pilipili hoho
- Vitunguu maji
- Chumvi
- Nyanya
- Ndimu
Maelekezo
- Menya ndizi na uhifadhi kwenye chombo chenye maji ili zisipate kubadilika rangi
- Andaa samaki – osha, kata vipande vinavyofaa au kama unapenda mpike
mzima – kamulia ndimu. Changanya samaki na limao. Kisha mhifadhi samaki
pembeni.
- Andaa nyanya – osha na kisha menya nyanya 3 na kuzikata vipande vidogo. Hifadhi kwenye chombo.
- Menya vitunguu maji 2 vikubwa halafu kata kwenye vipande vidogo unavyopendelea.
- Osha na kisha kata pilipili hoho 1 kubwa kwenye vipande vidogo. Fanya vivyo hivyo kwa carrots 1 kubwa
- Weka ndizi kwenye sufuria au kikaangio kinachofaa kupikia
- Weka vitunguu maji juu ya ndizi, halafu weka nyanya juu yake, kisha malizia na karoti.
- Weka samaki wako kwenye kikaangio kwa kuwapanga vizuri juu ya karoti.
- Nyunyizia chumvi ya kutosha. Usiongeze mafuta maana kwenye samaki na
vitunguu kuna mafuta ya kutosha, hivyo haina haja ya kuongeza zaidi.
- Weka maji kiasi kama kikombe 1 kikubwa halafu funika na mfuniko
usioruhusu mvuke kutoka. Hii inasaidia zile mboga mboga (karoti,
pilipili hoho, kitunguu na nyanya) zichuje maji yake na kukipa chakula
radha na harufu nzuri.
- Subiria kwa muda wa dakika 15 hadi 20 na mchemsho wako utakuwa tayari kuliwa.
Post a Comment