Mahitaji
- Unga wa ngano kilo 1.
- Sukari kijiko 1 cha chai.
- Mayai 2.
- Karoti 2.
- Kitunguu maji
- Chumvi ½ kijiko cha chai.
- Vanila
- Cream ya maziwa
- Maji
Maelekezo
- Weka unga wako kwenye chombo kikavu. Ongeza sukari na chumvi weka kidogo sana.
- Kwangua carrot zako ila zitoke zipande vidogo vidogo sana. Kata
vitunguu vipande vyembamba. Tenganisha vitunguu ili visije kushikana.
- Weka vitunguu na karoti kwenye unga. Koroga mchanganyiko na mikono (Hakikisha mikono yako ni misafi)
- Mchangayiko ukishakuwa sawia, ongeza maji kiasi kisha endelea
kukoroga unga. Angalia uwiano wake, usiwe mzito sana wala mwepesi sana.
Ongeza maji ili kupata mchanganyiko sawia.
- Pasua mayai na weka kwenye mchanganyiko kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe sawia.
- Weka cream ya maziwa kisha koroga vizuri.
- Weka ½ kijiko cha vanila kisha koroga. Vanila inahitajika kuongeza harufu, usiweke nyingi sana.
- Bandika kikaangio chako jikoni (frying pan). Ikipata moto, chota
mchanganyiko na weka kwenye kikaangio. Unaweza kutumia kikombe au upawa
kufanya zoezi hili.
- Weka rojo ya unga wako kwenye kikaangio chako (fryin pan) uwe na umbo la duara kama chapati.
- Ikikauka geuza na weka mafuta, kisha geuza upande wa pili angalia kama imeiva unatoa hapo tayari kwa kuliwa.
Post a Comment