Andaa vitunguu – pilipili hoho, kitunguu saumu na kitunguu maji –
menya na kata vipande vidogo. Ponda kitunguu saumu kwenye kinu.
Andaa nyama (samaki, kuku au ya ng’ombe) kwa kuikata vipande, kuiosha na kisha kuichemsha.
Weka ndimu na chumvi kwenye nyama.
Nyunyuzia pilipili manga
Usiongeze maji kwenye nyama. Acha ikauke.
Nyama ikikauka, weka kitunguu.
Loweka slice ya mkate kwenye maji. Itoe na ikamue kisha changanya na
mayai lililopasuliwa na kukorogwa na coriander. Hakikisha mchanganyiko
umejichanganya vizuri.
Injika kikaangio jikoni. Weka mafuta mengi kiasi. Subiria yachemke.
Tengeneza umbo la uviringo kutoka kwenye nyama,samaki au kuku kisha chovya kwenye rojo la mkate na mayai .
Tumbukiza mchanganyiko kwenye mafuta. Ingiza kimoja baada ya
kingine. Ili kupata matokeo mazuri, ingiza kwenye mafuta, huku ukitumia
mshikio, weka mchanganyiko ndani ya mafuta kwa muda wa sekunde 5 – 8 ili
kujenga koti na kuwezesha kuiva vizuri.
Rudia hatua hii kwa vipande vyote vilivyobaki.
Ipua vile vilivyoiva na subiria vikauke – unaweza kujiramba
Post a Comment