Jinsi ya Kupika Togwa - ChefMapishi.


Jinsi ya Kupika Togwa: 

Mahitaji:

  •     unga wa mahindi
  •     Maji mililita125
  •     Unga wa kimea cha mtama(mtama ulioteshwa ukaanikwa ukaenda kusagwa) nusu kikombe cha chai
JINSI YA KUPIKA:
  •     Pika uji mzito kwa kutumia unga wa mahindi.
  •     Uji ukiiva, epua na uache upoe hadi uwe wa vuguvugu.
  •     Koroga unga wa kimea kwenye maji kisha weka kwenye uji wenye ujazo wa lita mbili na nusu.
  •     Koroga mpaka kimea kichanganyikane vizuri na uji na kua mwepesi,
  •     Funika na acha togwa ichachuke usiku kucha au kwa masaa 12.
  •     Unaweza pia ukampa mtoto pale tu baada ya kupika ikipoa mana ina faida nyingi mwilini.
  •     Togwa inaweza kukaa siku nzima bila kuharibika. sasa unaweza kujiramba na wanafamilia.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post
Ads1
Ads2