Weka unga kwenye bakuli kisha ongeza sukari, chumvi, yai, maziwa ya
unga, butter na hiliki. Changanya viambato mpaka mchanganyiko uwe sawia.
Ongeza maji ya uvuguvugu kiasi kwenye mchanganyiko na uanze kukanda.
Ni vizuri kukanda mchanyiko huu kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha
donge lote la unga limelainika vizuri.
Gawanya unga uliokwandwa katika madonge manne (4) tofauti.
Weka unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze
kusukuma donge moja katika shape ya chapati. Katika kusukuma, hakikisha
unga wako uko wa wastani – siyo mwembamba sana wala mnene.
Ukimaliza kusukuma kata unga kutokana na umbo upendalo kupika
maandazi na uyatandaze katika ubao au sinia lililonyooka. Hakikisha
sinia au ubao umenyunyuziwa unga wa ngano ili kuzuia unga utakaoweka
usingandie.
Rudia hiyo hatua kwa madonge yote yaliyobakia.
Ukimaliza kuandaa maandazi yako, weka maandazi yako katika sehemu
iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka. Hii inaweza kuchukua hadi masaa 3
ili hamira kuumua vizuri unga wako.
Unga ukishaumuka, bandika sufuria, au kikaangio pamoja na mafuta
jikoni. Hakikisha mafuta ni mengi ili kuwezesha maandazi kuiva vizuri.
Mafuta yakishachemka tumbukiza mandazi. Acha maandazi kwenye mafuta mpaka yabadilike rangi na kuwa ya brown.
Maandazi yakishaiva, ipua na weka kwenye chujio ili kukausha mafuta. Rudia hatua hizi kwa maandazi yote yaliyobaki.
Post a Comment