Mahitaji:
- Unga wa ngano Kilo 1
- Hamira kijiko 1 cha chakula
- Chumvi 1/2 kijiko cha chai
- Sukari kijiko 1 kidogo cha chai
- Maziwa au tui bubu la nazi (Au vyote kwa pamoja)
- Uji mzito wa maboga ya njano yaliyochemshwa na kupoa kikombe kimoja cha chai (Siyo lazima)
- Vanila 1/2 kijiko kidogo cha chai
- Siagi kidogo.
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Maelekezo:
- Andaa maji ya uvuguvugu ujazo wa nusu kikombe kidogo cha chai.
- Weka hamira kwenye ya maji ya uvuguvugu kisha funika kwa muda wa dakika 3 hadi 5
- Andaa unga wa ngano. Chekecha ili kutoa uchafu ( kama una mchanyiko na vitu tofauti)
- Pasha moto sufuria ya kukandia
- Chemsha mafuta ya kula (mililita 20 – 30)
- Mimina hamira ( iliyoumuka kwenye maji) kwenye unga. Changanya vizuri kisha mimina mchanganyiko kwenye mafuta yanayochemka.
- Koroga kwa kutumia mwiko, japokuwa ni vizuri sana ukitumia mkono ( kuwa makini mafuta yasiwe ya moto sana)
- Ongeza maziwa au tui la nazi na endelea kukanda hadi unga uwe laini na usigandiane na sufuria
- Weka siagi kidogo kisha endelea kukanda.
- Weka vanilla kisha endelea kukanda. Vanilla inaleta harufu nzuri kwenye scones zako.
- Ukimaliza kukanda vizuri, paka sufuria mafuta, weka mchanganyiko wa unga uliokanda kisha funika na weka sehemu yenye uvuguvugu au joto kwa dakika 30 -45 ili unga uumuke vizuri. Joto liwe kati ya nyuzi 80°C hadi 120°C. Kama unatumia Oven ni vizuri kama utawasha ili lipate moto kabla ya kuweka mchanganyiko wa unga. Zima kabla ya kuweka mchanganyiko wako. Kisha weka mchanganyiko ili uumuke vizuri. Si lazima oven, unaweza kutumia jiko la mkaa lenye moto mdogo kiasi au jiko tofauti kwa kurekebisha kiwango cha joto.
- Mchanganyiko wa unga wenye hamira ukishaumuka vizuri, kanda tena kiasi na kisha gawa matonge madogo madogo (kutokana na umbo utakalo). Panga matonge kwenye mduara wa sufuria ambao umepaka mafuta (siagi) kisha weka kwenye sehemu yenye joto au vuguvugu kwa muda dakika 45. Joto liwe kati ya nyuzi 80°C hadi 120°C.
- Angalia kama unga umeumuka vizuri na kuongezeka kwenye sufuria. Weka moto kwenye jiko la mkaa ili liwe la moto kwa dakika 10 . Punguza moto na injika sufuria yenye scones juu ya jiko. Palia mkaa wenye jivu la moto juu ya mfuniko na subiri kwa dakika 10 kisha funua uangalie kama zimeiva. Kama bado ongeza moto wa jivu kidogo na subiri kwa dakika 5 zaidi.
- Ukifunua na kuona zimebadilika rangi na kuwa kahawia ( brown) zipake siagi kwa juu na funika. Baada ya dakika 2 mimina scones zako kwenye chombo kisafi na acha zipoe.
- Unaweza kujiramba na scones hizi kwa chai, maziwa, kahawa, vinywaji tofauti. Ni njia mbadala ya kuwapikia watoto wakiwa wanaenda shule ili kuweza kula wakati wa mapumziko, vilevile ni kitafunwa kizuri kwa wale wanaoenda kazini na hawana muda wa kula nyumbani.
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Post a Comment