Mahitaji
- Mchele kg 1
- Tui la nazi vikombe2
- Yai 1
- Sukari ½ kikombe
- Iliki kijiko 1 cha chakula iliyosagwa
- Unga wa ngano vijiko 2 vya chakula
- Mafuta ya kula
- Hamira ½ kijiko cha chai
Maelekezo
- Loweka mchele kwa muda usiopungua masaa 4, kisha chuja maji. Weka
mchele na tui la nazi kwenye blender. Saga pamoja ili mchanyiko ulainike
usiwe na chenga.
- Weka Iliki, hamira na unga wa ngano kwenye mchanganyiko ulio kwenye
blender. Saga pamoja hadi mchanyiko uwe uji uliochanganyika vizuri.
Mimina mchanganyiko kwenye bakuli. Funika vizuri kisha acha uumuke
kiasi, ukiumuka weka sukari na yai kisha changanya vizuri.
- Weka chuma cha kuchomea vitumbua jikoni, moto usiwe mkali sana. Weka
mafuta kidogo kwenye mashimo ya chuma cha kuchomea – kijiko baada ya
kingine. Mafuta yakipata moto, pakua uji kwa kutumia upawa kisha jaza
mashimo ya kukaangia virutumbua. Hakikisha kitumbua kinaiva vizuri na
kukauka kabla ya kugeuza upande mwingine. Weka mafuta upande wa pili wa
kitumbua, acha kikauke vizuri na kuwa na rangi ya kahawia. Toa kitumbua
na weka pembeni. Rudia hatua hii hadi uji wa vitumbua uishe.
- Tenga vitumbua na ujirambe. Unaweza kula vikiwa vya moto au vya baridi
Unaweza kula vitumbua na chai, kama kitafunwa kawaida au tofauti.
Post a Comment