Juisi ya Chungwa na Asali - ChefMapishi.

   
Juisi ya chungwa na asali – kinywaji cha moto

Ni kinywaji murua kwa wakati wa kupumzika jioni ukiwa unatafakari maisha. Ni kinywaji mbadala asubuhi kwa chai, maana hunywewa kikiwa cha moto na hakuna sukari inayoongezwa bali asali ambayo haina madhara mwilini. Kuwa makini maana asali huwa inakufanya upate usingizi kirahisi.

Mahitaji:

  •     Juice ya chungwa (Unaweza kukamua au ukatumia ya box)
  •     Asali ya nyuki
  •     Chombo cha kuchemshia ( sufuria, glass au bilauri)
  •     Microwave au jiko la kawaida
JINSI YA KUPIKA:
  •     Unaweza kuandaa juisi hii kwa kuchanganya asali na juisi na kisha kuipasha moto.
  •     Kama unatumia microwave changanya juisi na asali na kisha weka kwenye microwave kwa muda wa dakika 1 hadi 2 ili ipate kuchanganyika vizuri.
  •     Kama huna microwave, changanya asali na juisi kisha weka kwenye sufuria na bandika jikoni kwa muda wa dakika 5 hadi 7. Acha ichemke vizuri ili asali na juisi zichanganyike vizuri. Unaweza kukoroga pia ili kusaidia mchanganyiko uwe sawia.
  •     Asali ikiwa kwenye microwave inapata kulainika, hivyo huchanganyika vizuri na juisi na kuipa utamu wa kipekee. Kwa maana hiyo unaweza pia kutumia asali yenye mabonge maana italainika vizuri, kwani microwave pia hutumika kulainisha asali.

Tahadhari: Kama unatumia microwave hakikisha hutumii sufuria au kitu chochote cha bati (kijiko, uma, kisu nk) maana ni hatari na unaweza kusababisha mlipuko. Ni vizuri kama utatumia bakuli za udongo au glass kutengeneza huu mchanganyiko.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post
Ads1
Ads2