Mchuzi wa Nazi na Mbuzi - ChefMapishi.


Mahitaji:

  • Mdalasini vijiti 3
  • Hiliki punje 5
  • mbegu za pilipilimanga 5
  • Vitunguu 2 vikubwa vilivyokatwakatwa vipande
  • Vitunguu Saum na tangawizi vilivyosagwa vijiko2
  • Bay leaf 2
  • Nyama ya mbuzi nusu
  • Tui la nazi zito vikombe viwili na nusu
  • Chumvi
  • Curry powder kijiko cha chai 1
  • Mafuta au samli vijiko viwili vya chakula
  • Mvuje majani 5(sio lazima)
  • Maji kidogo

JINSI YA KUPIKA:

  1. Chukua nyama yako ioshe vizuri ikate kate ukubwa unaopenda weka chumvi curry powder mchanganyiko wa vitunguu Thom kijito kimoja iache nusu saa ikolee viungo,baada ya nusu saa.
  2. Chukua karai lako weka hiliki kaanga bila mafuta toa weka pembeni, weka pilipili manga kaanga toa weka mdalasini kaanga toa, weka bay leaf kaanga toa (hakikisha vyote unakaanga bila mafuta yaani unapasha moto tu na weka kimoja utoe ndio ueke chengine na hakikisha huunguzi)
  3. Chukua sufuria lako weka jikoni weka mafuta eka viungo vyako pamoja na majani ya mvuje weka vitunguu maji weka mchanganyiko wa Thom acha kidogo halafu weka nyama yako ichanganye vizuri weka maji kidogo
  4. Halafu weka tui lako huku unagoroga, onja chumvi kama kidogo ongeza acha tui lichemke mpka liive Mchuzi wako utakuwa tayari.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post
Ads1
Ads2