Vipimo:
Nyama ya mbuzi ya mafupa au ya ng'ombe - Kilo moja
Mafuta - 2 vijiko vya supu
Vitunguu maji (vikate vidogo vidogo) - 2
Nyanya (kata ndogo ndogo) - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari ya pilau ya unga (Jeera) - 1 kijijo cha chai
Gilgilani ya unga (Dania) - ½ kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga - ¼ kijiko cha chai
Kotmiri (iliyokatwa ndogo ndogo) - kiasi
Nanaa (iliyokatwa ndogo ndogo) - kiasi
Chumvi - kiasi
Siki - 3 vijiko vya supu
Shayiri* /Hariys - 2 vikombe
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
* Shayiri ni aina ya ngano (oats) ila ni tofauti kidogo na ngano. Baadhi ya maduka inajulikana kama ni 'hariys' .
Kidokezo:
Ikiwa shayiri nzima nzima, basi roweka kwa muda wa masaa na uchemshe mpaka ziive.
Namna ya kutayarisha na kupika
- Chemsha nyama na chumvi kwa maji kiasi mpaka iwive.
- Katika sufuria nyengine, weka mafuta na kaanga vitunguu kidogo tu vilainike, usiviwache kugeuka rangi.
- Weka bizari zote, pili pili manga, chumvi.
- Tia thomu na tangawizi.
- Tia nyanya na bila ya kuzikaanga sana tia nyama na supu yake.
- Tia kotmiri, nanaa.
- Pembeni changanya shayiri na maji koroga kisha tia katika supu.
- Iwache ichemke kidogo tu ngano ziwive.
- Tia siki na tayari kuliwa.
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Post a Comment