Pilau Ya Nyama Na Mtindi
VIPIMO:- Nyama iliyokatwa vipande - 1 Ratili(LB)
- Mchele Basmati - 2 Magi
- Chumvi ya wali - kiasi
- Kitungu kilichokatwa katwa - 1 kikubwa
- Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu
- Mtindi (yogurt) - ½ kikombe
- Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari - 2 vijiko vya supu
- Mafuta kidogo yakukaangia
- Rangi ya manjano (ukipenda)
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA:
- Osha mchele na roweka nusu saa .
- Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).
- Tia saumu na tangawizi na ukaange kidogo.
- Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga nyama isiwe nyekundu tena.
- Tia maji gilasi 1½- 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.
- Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.
- Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.
- Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza rangi (ukipenda) kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.
- Changanya wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa.
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Post a Comment