Jinsi ya Kupika Pilau Ya Nyama Ng'ombe Na Nyanya.
Vipimo.- Mchele (Basmati) - 3 vikombe
- Nyama ya ngo’mbe - 1 kg
- Pilipili boga - 1 kubwa
- Nyanya - 2 kubwa
- Vitunguu maji - 2 vikubwa
- Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
- Tangawizi - 1 kijiko cha chai
- Ndimu - 1
- Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
- Mdalasini - ½ kijiko cha chai
- Binzari nyembamba - 1 kijiko cha chai
- Pilipili manga - ½ Kijiko cha chai
- Hiliki - ½ Kijiko cha chai
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Roweka mchele wako katika chombo
Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi
Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi
Katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni
Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia
Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto
Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya
Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi
Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke
Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza
Funika na punguza moto na uache uive taratibu
Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Post a Comment