Mahitaji;
Kuku na mbogamboga (unaweza tumia mboga tofauti)
- 350g minofu ya kuku
- Vijiko 2 vya chakula mafuta ya mzaituni
- Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
- Kijiko 1 cha chai tangawizi
- Karoti 1 kubwa
- ½ pilipili hoho nyekundu
- Kikombe 1 maharagwe machanga
- Kikombe 1 uyoga
- ½ kikombe majani ya kitunguu
- ¼ kikombe korosho
- Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
- Mbegu za ufuta kunyunyizia juu
Sosi;
- Kijiko 1 cha chakula siki (red wine vinegar)
- Kijiko 1 cha chakula sosi ya soya
- Kijiko 1 cha chakula mafuta ya ufuta
- Kijiko 1 cha chakula kitunguu samu na tangawizi
- Kijiko 1 cha chakula maji ya ndimu
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Maelekezo;- Twanga kitunguu saumu na tangawizi; kamua maji limao
- Osha, kausha na katakata nyama vipande virefuvirefu. Changanya nyama na kijiko 1 cha chai tangawizi, kijiko 1 cha chai kitunguu saumu, pilipili manga na chumvi kwa kuonja
- Kwenye kibakuli kidogo, changanya viungo vyote vya sosi, weka pembeni
- Katakata mbogamboha vipande virefuvirefu; katakata majani ya kitunguu vipande vidogovidogo
- Kwenye kikaangio katika moto mkali kiasi, chemsha kijiko 1 cha mafuta ya mzaituni
- Ongeza kuku mwenye viungo, kaanga mpaka aive; kama dakika 3-4. (Hakikisha hujazi sana kikaangio, acha kuku aive kwa nafasi. Endapo unatumia kikaangio kidogo, pika nusu nusu)
- Kuku akiiva, hamishia kwenye sahani
- Rudisha kikaangio kwenye moto, ongeza kijiko 1 cha chakula cha mafuta yaliyobakia katika moto wa juu kiasi. Ongeza karoti na maharagwe machanga, pika kwa dakika 1 hadi 2
- Ongeza uyoga na pilipili hoho. Pika kwa dakika moja nyingine (au mpaka ziive kama unavyopenda wewe)
- Rudisha kuku kwenye kikaango, changanya vizuri
- Mimina mchanganyiko wa sosi
- Ongeza korosho na majani ya kitunguu, pika kwa sekunde kama 30
- Ipua, nyunyizia mbegu za ufuta. Pakua cha moto
Mpendwa
Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO
UPISHI. Sasa
inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Post a Comment