Pilau ya Mboga Mboga - ChefMapishi.

Mahitaji:

  • Mchele wa kupikia biriyani.
  • Bizari nyembamba
  • Njegere
  • Giligiliani
  • Kitunguu maji
  • Nyanya 3
  • Tangawizi 1
  • Vitunguu swaumu 2
  • Viungo vya pilau (chaguo lako)
  • Karafuu
  • Pilipili manga
  • Karoti
  • Pilipili hoho
  • Kolimaua
Mpendwa Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO UPISHI.  Sasa inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.

Maelekezo:

  • Menya vitunguu maji na kata kufuatisha uviringo wake ili upate umbo la mduara kisha weka kwenye chombo.
  • Osha nyanya na kata vipande vinne kwa kila nyanya
  • Osha karoti na kisha zimenye. Kwangua kiasi na nyingine kata vipande vidogo.
  • Osha na kisha kwangua kiasi cha karoti na nyingine kata vipande vidogo.
  • Osha kolimaua na itoe kwenye shina ili upate maua yake.
  • Osha giligiliani na kuikata
  • Osha na weka nyegere kwenye chombo chenye maji.
  • Menya tangawizi na kisha ikwangue
  • Menya vitunguu saumu kisha uvitwange.  
  • Andaa viungo vyote vya pilau pembeni tayari kutumika
  • Osha na kisha andaa karafuu na pilipili manga
  • Injika sufuria jikoni.
  • Weka mafuta ya kupikia. Weka viungo vya pilau vya unga kisha weka bizari nyembamba na kaanga kwa muda kiasi.
  • Weka kitunguu saumu – koroga kiasi. Weka tangawizi na endelea kukoroga. Weka kitunguu maji kisha koroga kwa muda kiasi. Acha viive kabla na kuanza kubadilika rangi.
  • Weka nyanya, chumvi, na pilipili manga. Koroga na kisha acha vichemke kwa dakika chache.
  • Weka karafuu, karoti, pilipili hoho, kolimaua na njegere. Endelea kukaanga kwa muda wa dakika kama 10.
  • Weka mchele huku ukiendelea kukaanga ili mchele wako uchanganyike vizuri na viungo kwenye sufuria.
  • Weka maji kulingana na kiasi cha mchele wako.
  • Weka moto wa wastani na kisha funika sufuria chakula kiive. Baada ya dakika 10 au 15 geuza pilau lako kisha weka majani ya giligiliani ili kuongeza ladha na harufu nzuri ya chakula. Funika chakula ili kiendelee kuiva.
  • Subiria kwa muda wa dakika 10 na chakula kitakua tayari kuliwa.
Mpendwa Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO UPISHI.  Sasa inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post
Ads1
Ads2