Kupika Keki ya Nanasi - ChefMapishi.

Mahitaji:

  • Nanasi lililoiva vizuri liwe tamu kata slice
  • Butter nusu kikombe cha chai
  • Sukari ya brown nusu kikombe 
  • Juice ya nanasi vijiko 4 vya chakula
  • Unga ngano vikombe 2
  • Baking powder kijiko 1 na nusu cha chai
  • Chumvi nusu kijiko cha 1
  • Sukari nyeupe vikombe 2
  • Mayai 3
  • Mdalasini kijiko 1cha chai
  • Vanilla kijiko 1 cha chai
  • Butter kikombe 1
  • Maziwa nusu kikombe 
  • Cherries

Mpendwa Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO UPISHI.  Sasa inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.

Maelekezo:

  • Washa jiko, bandika sufuria au chombo utakachopenda kuokea keki  weka butter iyeyeyuke, weka sukari ya brown isambaze juu.
  • Chukua slice za nanasi vipange juu ya mchanganyiko, chukua cherries weka kwenye nanasi yaani katikati ya kile kipande cha nanasi.
  • Epua weka pembeni, chukua bakuli weka unga, chumvi, mdalasini na baking powder changanya vizuri weka pembeni.
  • Chukua bakuli weka butter, weka sukari nyeupe koroga mpaka ilainike kisha ongeza mayai koroga, weka maziwa, vanila na juice ya nanasi.
  • Koroga kisha weka mchanganyiko ule wenye unga huku ukiendelea kukoroga vichanganyikane vizuri.
  • Mchanganyiko uwe mzito ila sio sana. Chukua mchanganyiko wenye unga weka kwenye ule wenye butter na nanasi, sambaza vizuri kisha oka kwa dakika 40.
  • Epua acha ipoe kwa dakika 5, anza kujiramba na familia.
Mpendwa Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO UPISHI.  Sasa inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Bonyeza Dole hapo chini.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post
Ads1
Ads2