Chukua graham cracker weka kwenye blenda na sukari vijiko 2, saga mpaka ilainike. Pima vikombe 2
Chukua bakuli weka graham cracker uliyosaga weka na butter koroga
ichanganyike vizuri kisha weka kwenye chombo cha kuokea, weka na cubes
za caramel oka kwa dakika 30.
Itoe iache ipoe, chukua bakuli weka cream cheese, mayai, vanila,
sukari na unga vijiko 2 changanya mpaka ilainike vizuri, kisha mwagia
kwenye ule mchanganyiko ulio uoka mwanzo.
Chukua caramel weka maziwa bandika jikoni weka moto mdogo sana. Kisha mwagia juu ya ule mchanganyiko.
Oka kwa dakika 45 itoe, iache ipoe kwa dakika 15,kisha mwagia caramel iliyobaki kwa juu kisha kata wape watu wajirambe.
Post a Comment