Kuku Mboga wa Majani - ChefMapishi.



Mahitaji:
  • Minofu ya kuku ½ kilo
  • Kitunguu saumu
  • Chumvi kijiko 1 cha chai
  • Limao au ndimu 1
  • Pilipili hoho – kijani, njano na nyekundu
  • Pilipili manga
  • Curry powder
  • Tangawizi 1
  • Vitunguu maji 2
  • Olive oil
Mpendwa Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO UPISHI.  Sasa inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.

Maelekezo:

  • Leo tunaandaa nyama ya kuku itakayokuwa kama hivi ikishaiva
  • Kata minofu ya kuku kwenye vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kuiva.
  • Nyama hii haichemshwi bali inaanza kukaagwa moja kwa moja, hivyo vipande vidogo vidogo vinasaidia kuifanya iive vizuri hadi ndani.
  • Osha nyama vizuri. Weka kwenye chombo kikavu.
  • Nyunyuzia chumvi. Koroga.
  • Nyunyuzia limao, kisha koroga zaidi.
  • Weka tangawizi iliyopondwa ili kuipa nyama ladha nzuri. Acha nyama ikae kwa dakika 5 hadi 7 ili limao lipate kuingia.
  • Wakati nyama inakolea limao. Kata kitunguu maji kwenye vipande vidogo, kisha weka kwenye chombo pembeni.
  • Kata pilipili hoho kwenye vipande virefu kiasi. Weka kwenye chombo pembeni.
  • Kata karoti kwenye vipande vidogo. Weka kwenye chombo pembeni.
  • Weka kikaangio jikoni, ongeza mafuta ya olive. Acha yapate moto kiasi
  • Weka nyama jikoni. Koroga kiasi kisha acha iive vizuri hadi ianze kubadilika rangi kuwa ya rangi ya udongo.
  • Weka pilipili manga juu ya nyama. Nyama ikiwa tayari ipua kisha hifadhi pembeni.
  • Weka mafuta kwenye kikaangio. Subiri yapate moto kisha weka vitunguu.
  • Weka kitunguu saumu. Koroga vizuri acha viive pamoja na vitunguu maji.
  • Weka pilipili hoho, koroga mchanganyiko. Baada ya dakika moja weka karoti na endelea kukoroga. Acha viive kwa dakika 3 hadi 5.
  • Weka nyama ya kuku iliyoiva kwenye mchanganyiko wa mboga za majani.
  • Ongeza curry powder, koroga mchanganyiko vizuri. Funika na mfuniko. Acha ichemke vizuri. Takribani dakika 5 hadi 7.
  • Ipua mboga yako na iko tayari kuliwa
  • Unaweza kula na wali, ugali, ndizi, viazi, chapati na vinginevyo vingi. Chaguo ni lako.
Mpendwa Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi MAFUNZO UPISHI.  Sasa inapatikana Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post
Ads1
Ads2